Matthew 1:1-17

Kumbukumbu Za Ukoo Wa Yesu Kristo

(Luka 3:23-38)

1 aHabari za ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Abrahamu:

2 bAbrahamu akamzaa Isaki,
Isaki akamzaa Yakobo,
Yakobo akawazaa Yuda na ndugu zake,
3 cYuda akawazaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari,
Peresi akamzaa Hesroni,
Hesroni akamzaa Aramu,
4Aramu akamzaa Aminadabu,
Aminadabu akamzaa Nashoni,
Nashoni akamzaa Salmoni,
5 dSalmoni akamzaa Boazi, na mama yake Boazi alikuwa Rahabu,
Boazi akamzaa Obedi, ambaye mama yake alikuwa Ruthu,
Obedi akamzaa Yese,
6 eYese akamzaa Daudi ambaye alikuwa mfalme.

Daudi akamzaa Solomoni, ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria.
7 fSolomoni akamzaa Rehoboamu,
Rehoboamu akamzaa Abiya,
Abiya akamzaa Asa,
8Asa akamzaa Yehoshafati,
Yehoshafati akamzaa Yoramu,
Yoramu ndiye Yehoramu, maana yake ni Yehova yu juu.

Yoramu akamzaa Uzia,
9Uzia akamzaa Yothamu,
Yothamu akamzaa Ahazi,
Ahazi akamzaa Hezekia,
10 hHezekia akamzaa Manase,
Manase akamzaa Amoni,
Amoni akamzaa Yosia,
11 iwakati wa uhamisho wa Babeli, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake.

12 jBaada ya uhamisho wa Babeli:
Yekonia alimzaa Shealtieli,
Shealtieli akamzaa Zerubabeli,
13Zerubabeli akamzaa Abiudi,
Abiudi akamzaa Eliakimu,
Eliakimu akamzaa Azori,
14Azori akamzaa Sadoki,
Sadoki akamzaa Akimu,
Akimu akamzaa Eliudi,
15Eliudi akamzaa Eleazari,
Eleazari akamzaa Matani,
Matani akamzaa Yakobo,
16 knaye Yakobo akamzaa Yosefu ambaye alikuwa mumewe Maria, mama yake Yesu, aitwaye Kristo.
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.


17Hivyo, kulikuwepo na jumla ya vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi hadi wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli, na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli hadi Kristo.

Copyright information for SwhNEN